Kundi la Yamoto Band limeingiza sokoni bidhaa za nguo zenye jina la kundi hilo ambapo zimeanza kuuzwa maeneo tofauti hapa jijini Dar es Salaam pamoja na baadhi ya mikoa hapa nchini.

Mkurugenzi wa Band hiyo, Said Fela ‘Mkubwa Fela’ amewataka mashabiki wa muziki kusubiria mambo makubwa kutoka katika brand ya Yamoto Band huku akiwata mashabiki hao kuchangamkia nguo mpya za brand hiyo ambazo zimeingia sokoni hivi karibuni.

Mkubwa Fela amesema nguo za brand ya Yamoto Band tayari zimeingia sokoni na zinapatikana katika maduka mbalimbali kwa hiyo wapenzi na mashabiki wa kundi hilo wajitokeze kuisapoti bidhaa hiyo.

Fela amesema kuwa kuna mambo mengi yanakuja, tuombe uzima lakini kwasasa tunazungumzia mzigo mpya ambao umeingia sokoni, nguo ni nzuri tunahitaji sapoti za mashabiki wetu katika kutuungisha.

Yamoto Band
Yamoto Band

Pia Fela amesema tayari ameshasajili logo ya brand ya Yamoto Band ili kukabilina na watu ambao watajaribu kutengeneza bidhaa feki.

Yamoto Band ni kundi lililojizolea umaarufu mkubwa hapa nchini kutokana na kazi zao kugonga vichwa vya mashabiki wao.

Kundi hilo linamilikiwa na Mkubwa Fela ambapo wiki iliyopita alizionesha nyumba alizowajengea wasanii hao ambapo ni moja ya mafanikio ya kundi hilo la muziki wa Bongo fleva hapa nchini.

Kundi hilo linaundwa na wasanii wanne ambao ni Dogo Aslay, Enock Bella, Beka na Maromboso.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *