Mwaka 2015 hakuna mpenzi wa burudani ya muziki Bongo ambaye hakuna anawajua YAMOTO Band.

Na katika hali ya kushangaza kidogo, YAMOTO Band walikuwa ni sehemu ya kampeni ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, rais John Pombe Magufuli.

Hiyo inaonyesha ni kwa kiasi gani YAMOTO waliweza kukonga nyoyo za mashabiki pamoja na kutengeza profile ambayo hata viongozi wa juu waliamini inaweza kuwasaidia kwneye kufanikisha mambo yao.

Lakini mwaka 2016, haukuwa mzuri sana kwa kundi hili la vijana wanne halikuwa na mafanikio makubwa kwenye kazi zao huku tetesi zikizagaa kuwa wamedhulumiwa na menejimenti yao iliyo chini ya Mkubwa Said Fella.

Tetesi ambazo zilivuma zaidi ni suala la kutapeliwa nyumba walizodaiwa kujengewa na menejiment yao lakini hata hivyo hakuna aliyeweza kuzithibitisha au kuzikanusha.

Je, hawakuwa na mahusiano mazuri na Mkubwa Fella? Ndio, kwa muda fulani walikosana na MKUBWA ingawa hakuna details ambazo zimetolewa juu ya hasa kile walichokosana.

Lakini kwa sasa, YAMOTO Band wamerudi tena mikononi mwa Mkubwa na Wanawe na wenyewe wanakiri kuwa ‘HILI NI JAMBO AMBALO HUKUWA UNALIFAHAMU’ Fella ndiye anayeweza kuwapoteza kwenye muziki kwasababu yeye ndiye aliyewafikisha hapo.

Will Yamoto Band blossom like never before?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *