Mkali wa Bongo Fleva, Y Tony ameendelea kuweka hisia zake wazi kwa mrembo kutoka Bongo Movie, Kajala Masanja.

Y Tony amesema kuwa uwepo wa Kajala ni moja ya sababu za kumfanya yeye kuendelea kujitahidi kufanya muziki mzuri kwenye industry ya Bongo Fleva.

Kajala Masanja
Kajala Masanja

Mwanamuziki huyo ambaye anatamba na wimbo wa Safina amesema kuwa Kajala anamu-inspire sana na anamuombea kwa Mwenyenzi Mungu azidi kuwepo ilimradi azidi kufanya vitu vizuri.

Y Tony ameendelea kusema kuwa katika wasanii wote wa kike ndiye msanii anayempenda kutoka kwenye moyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *