Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amezindua ujenzi wa Mji wa Safari pamoja na kuwapa hati  wakazi 100 wa mji wa Arusha.

Safari City ni mji wa kisasa uliopangwa vizuri kwa kufuata sheria na kanuni za mipango miji uliopo Jijini Arusha.

Eneo hili limepangwa viwanja vya nyumba za makazi, ofisi, biashara, hoteli, shule na viwanda vidogo vidogo.

Viwanja hivi vina huduma zote muhimu kama vile miundombinu ya maji, umeme, barabara na mfumo wa maji taka.

Mauzo ya viwanja hivi yanakwenda sambamba na mauzo ya nyumba za mfano ambapo viwanja vya makazi vinaanzia Tsh 7M na kuendelea.

Katika ziara hii Waziri Lukuvi alipokea taarifa ya ufutwaji wa mashamba kumi na mbili (12) yaliyoko Halmashauri ya Meru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *