Msanii na producer Wyclef Jean ametoa malalamiko yake baada ya polisi kumfananisha na mtuhumiwa aliyekuwa anatafutwa na kumfunga pingu kimakosa.

Wyclef na watu wawili akiwemo meneja wake walikamatwa na kuwekwa sero mjini Los Angeles baada ya polisi kupewa taarifa kuwa gari lililofanya ujambazi eneo flani limefanana na gari walilokuwa wanaendesha mastaa hao.

Wyclef anasema alikuwa amevaa kilemba cha bendera ya Haiti na polisi walimkamata sababu mmoja wa majambazi hao alitajwa akuwa amevaa kitamba cheusi kichwani.

Wyclef ametoa malalamiko hayo kupitia IG yake na kusema ni ubaguzi wa rangi kwa kitu alichofanyiwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *