Wanamiereka, Alberto Del Rio na Paige wamesimamishwa kwa muda kushiriki michezo hiyo baada ya kukiuka sera za shirika la wanamiereka la WWE.

WWE halijatoa maelezo kuhusu kufungiwa kwao lakini sera ya shirika hilo inasisitiza kuhusu umuhimu wa kutohusisha mchezo huo na mihadarati.

Ni mara ya kwanza kwa wana miereka hao maarufu kukiuka sheria za WWE.

Paige: Baada ya kushinda mkanda wa WWE.
Paige: Baada ya kushinda mkanda wa WWE.

Wote wawili wamesimamishwa kwa mda wa siku 30 na watakosa mashindano ya wikendi ya Brooklyn katika mji wa New York nchini Marekani.

Kati yao hakuna aliyezungumza kuhusu kusimamishwa kwao ambapo ilitolewa siku ya kuzaliwa kwa Paige.

Baadhi ya mashabiki wameonyesha kuhuzunishwa na marufuku hiyona lakini wengine wamesema kuwa kifungo hiko ni njama ya kupunguza umaarufu wa wanamiereka hao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *