Wolper azungumzia sakata la Kizz Daniel

0
71

Muigizaji wa Bogo Movie, Jacqueline Wolper  amezungumzia sakata la mwanamuziki, Kizz Daniel kutofanya shoo ya Summer Amplified iliyotakiwa kufanyika jijini Dar es Salaam.

Wolper ameonyesha kufurahishwa na kitendo cha hit-maker huyo wa ngoma ya Buga inayofanya vizuri kupitia mitandao ya kijamii kuingia mitini huku mashabiki wakipiga miayo ya kumsubiri ukumbini.

Kupitia Instastory yake, Wolper ameweka picha ya Kizz Daniel na kuandika; “Nafurahi ulichofanya jana maana hata ndoa zilitaka kuvunjika watu wamerudi asubuhi bwana Buga lakini bila kusahau wadada wamekopa na kukopwa kwa ajili ya nguo mpya na mawigi mapya, watu walijipanga kusema ukweli nimependaa hahahaha nakojoa jamani,” ameandika Wolper.

Inaelezwa kuwa, Kizz aligoma kufanya shoo hiyo kwa sababu ya kutokuwepo nguo zake ambazo kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ni kuwa alisahau nguo hizo nchini Kenya.

Pia, inadaiwa kuwa hata cheni yake aliyopanga kuivaa aliisahau Nigeria hivyo akagoma kupanda jukwaani kutokana na kukoseakana kwa vitu vyake hivyo muhimu.

LEAVE A REPLY