Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amesema kuwa ameachana rasmi na mpenzi wake ambaye ni msanii wa muziki kutoka ‘WCB’ Harmonize.

Wolper ambaye ni mkubwa kiumri na Harmonize amesema kwamba yeye na Harmonize, mapenzi yao yamekwisha kabisa hawapo pamoja kama zamani.

Muigizaji huyo amesema kuwa ameamua kuwa katika uhusiano kuna kugombana kukoseana na kusameheana mara nyingi, sasa wmeamua kila mtu aendelee na maisha yake.

Pia Wolper amesema kuwa hawezi kujutia uamuzi huo na moyo wake umeshazoea kwasababu alimkuta akiwa Wolper na wameachana akiwa Wolper labda kama angekuwa amenikuta Fatuma na kunifanya kuwa Wolper.

Vile vile Wolper ameongeza kwa kusema kuwa “Wakati tukiwa kwenye uhusiano wetu hatujawahi kusaliti au inawezekana tulichiti na tukasameheana ila kwangu ni rahisi kusamehe kwa kuchiti kuliko kukusamehe kwenye kosa dogo’.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *