Staa wa Bongo movie, Jacqueline Wolper amejiunga rasmi na Chama tawala CCM baada ya kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo “CHADEMA” ambapo alikuwa mwanachama wa chama hiko.

Muigizaji huyo alitangaza kujiunga na chama hicho tawala Jumamosi iliyopita kwenye mkutano mkuu uliofanyika Dodoma ambapo pia Rais Dkt John Magufuli alichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya akichukua nafasi ya Dk Jakaya Kikwete.

Wolper alikuwa akimuunga mkono aliyekuwa mgombea urais kupitia tiketi ya Ukawa, Edward Lowassa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba mwaka jana na Rais Magufuli kuibuka na ushindi.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Wolper aliweka picha ikimuonesha akimpa mkono Rais mstaafu, Dk Jakaya Kikwete kwenye mkutano jijini Dodoma.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *