Muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa hawezi kukataa salamu kutoka kwa aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, Harmonize.
Jacqueline Wolper amefunguka hayo baada ya kuonekana kusalimiana na ex wake huyo katika sherehe ya Diamond iliyofanyika Oktoba 2 mwaka huu.
Katika sherehe hiyo Wolper alionekana akisalimiana na Harmonize kitu ambacho kiliibua maswali kwa baadhi ya watu kutokana na wawili hao kuachana na kila mmoja ana mpenzi mpya ambapo Wolper yupo na Brown huku Harmonize akiwa na Sarah.
Jacqueline ameeleza kuwa jambo la yeye kumsalimiana na Harmonize halikuwa tatizo kwani salamu haikataliwa japokuwa wameshachana.
Pia Wolper amedai kuwa hakutokea na mpenzi wake huyo katika sherehe hiyo kwani alikuwa anaumwa kwa takribani siku tano na kuhusu kufutwa kwa picha zake mtandao wa kijamii wa Instagram, mrembo huyo amedai hafahamu kuhusu ilo kwani hajaingia katika mtandao huo.