Mshindi wa tuzo la Nobel raia wa Nigeria, Wole Soyinka, ametimiza ahadi yake baada ya kuichana green card yake.

Mwezi uliopta mshindi huyo wa tuzo la fasihi alisema kuwa angeirarua green card, ambayo humpa mtu kibali cha kuishi nchini Marekanai ikiwa Dionald Trump angechaguliwa kuwa rais wa Marekani.

Amesema hayo katika jiji la Johannesburg kuwa kutokana na vile Trump ameshinda, basi ametekeleza alichokisema

Soyinka amesema kuwa “Tayari nishafanya, nimetoka Marekani , nimefanya kile nilisema ningekifanya, nilitupa green card yangu , nimerudi ninapostahili,”.

Hata hivyo Soyinka hawashauri watu wengine kufuata mkondo huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *