Mkali wa muziki kutokea pande za Nigeria, Wizkid amesema kuwa anatarajia kufanya mambo makubwa mwaka 2017 kwani hawezi kuangalia aliyoyafanya mwaka 2016 kwani yashapita tayari.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 26, alifanya makubwa mwaka 2016, kwa kufanya kazi na nyota wakubwa wa muziki duniani akiwemo, Drake na Chris Brown.

Kupitia akaunti ya Instagram mkali huyo amesandika kuwa “Mwaka jana nilifanya makubwa pamoja na kununua nyumba nchini Marekani, lakini mafanikio hayo si kitu chochote kwangu, natarajia kufanya makubwa zaidi kwa mwaka huu.

Pia akaongeza kwa kuandika “Kwa sasa nipo katika mapumziko hadi Februari mwaka huu, sina mpango wa kuangalia nilipotoka, nataka niwe kama nimezaliwa upya huku nikiwa na kiu ya mafanikio,”.

Wizkid ni mwanamuziki bora kwasasa barani Afrika kutokana na kazi zake muziki mpaka ikampelekea kushinda tuzo nne kwenye tuzo za MTV MAMA Afrika zilizofanyika jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini Oktoba mwaka jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *