Wizkid asitisha kuachia albam mpya

0
238

Mwanamuziki wa Nigeria, Wizkida amesitisha kuachia Album yake mpya Made In Lagos ambayo ilikua inatarajiwa Kutoka Siku ya Jana Oktoba 15 , ili kupisha Maandamano yanayoendelea nchini humo ya Kupinga Unyanyasaji wa Polisi.

Kupitia Ujumbe aliopost Katika Ukurasa wake wa Instagram, Wizkid amesema kuwa anadhani si sahihi kwa hivi sasa kuachia Album katika kupindi Muhimu kama hichi ambacho watu wanapigania haki zao nchini Nigeria.

“Kutokana na hali ilivyo sasa Nigeria na kila kitu kinachoendelea . Nimefikia Maamuzi ya kupeleka mbele Album yangu hivyo itatoka tarehe nyingine.

Nawaomba radhi Mashabiki zangu ambao nitawaangusha kwa hilo , Lakini nadhani huu si muda sahihi kuachia Album ” – ameandika.

LEAVE A REPLY