Baada ya mwanamuziki wa Nigeria, Wizkid kuachia wimbo wake mpya ‘African Bad Gyal’ kufanya vizuri kwenye vyombo mbalimbali vya habari, msanii huyo ameweka wazi kuwa anabebwa vizuri na mkali wa RnB nchini Marekani, Chris Brown.

Wimbo huo, ambao umeachiwa wiki iliyopita, huku akimshirikisha msanii huyo, unaonekana kufanya vizuri kwa kipindi kifupi ndani na nje ya Nigeria, hivyo anaamini ushirikiano wa Chris unazidi kumfanya awe juu.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Afrikan Bad Gyal ni wimbo ambao unaweza kupigwa sehemu yoyote, ninashukuru kuona unafanya vizuri”.

Pia amesema kuwa “Chris Brown amezidi kuupa nguvu wimbo huo, japokuwa si mara ya kwanza kufanya naye kazi, lakini safari hii ameonekana kunipa nguvu zaidi, nawashukuru sana mashabiki wangu kwa sapoti wanayonipa,”.

Mwanamuziki huyo kwasasa anafanya vizuri ndani na nje ya Afrika kutokana na kufanya nyimbo na wasanii wakubwa nchini Marekani kama Drake na Chris Brown.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *