Baada ya Roma Mkatoliki na wenzake kutekwa na kuchukuliwa na watu wasiojulikana kwenye studio za Tongwe zilizopo Masaki jijini Dar es Salaam wizara ya habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo yatoa neno.

Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo ambayo iko chini ya Dr. Mwakyembe imetoa taarifa ifuatayo.

Taarifa hiyo imesema kuwa  “Kwa dhamana yake katika tasnia ya Sanaa, Wizara imepokea kwa mshtuko taarifa za kutoweka kwa Mwanamuziki Ibrahim Mussa kwa jina la kisanii “Roma”.

 Wizara imefuatilia kwa karibu suala hili kwa kuwa lina muelekeo wa jinai kutokana na taarifa kutoka vyombo vya dola zinathibitisha kuwa Roma Mkatoliki hashikiliwi katika kituo chochote cha polisi.

 Wizara inawaomba wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa zozote zitakazo saidia kujua alipo msanii huyo.

 

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *