Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea magari 58 kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA).

Who imetoa msaada wa magari 50 ya kubebea wagonjwa (Ambulance) na UNFPA imetoa magari manane ambayo yatatumika kuratibu shughuli za afya ya mama na mtoto.

Waziri anayeshughulikia wizara hiyo, Ummy Mwalimu amesema yatagawiwa katika mikoa sita iliyopo Kanda ya Ziwa.

Mwalimu amesema mikoa hiyo ilionekana kuwa na utumiaji mdogo wa huduma ya uzazi wa mpango, wanawake wachache ndio waliojifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya na kuna idadi kubwa ya vifo.

Pia amewataka waganga wakuu wa mikoa ambao watakabidhiwa magari hayo kuyakatia bima ya ajali ili yaendelee kudumu kutoa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake mwakilishi Mkazi wa UNFPA-Tanzania, Dk. Hashina Begum, alisema magari hayo manane waliyoyatoa yana thamani ya Sh milioni 387.

Naye Mkurugenzi Mkazi wa WHO, Dk. Grace Saguti, alisema ambulance hizo zilizotolewa zitakuwa na huduma zote muhimu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *