Staa wa Bongo Fleva, Jux ameachia rasmi ngoma yake mpya WIVU.

WIVU ni ngoma inayoifuatia One More Night ambayo inaendelea kukimbiza kwenye soko la muziki wa Bongo Fleva.

Ngoma hiyo imezinduliwa kupitia kituo cha redio cha Clouds Fm.

Jux ameendelea kuwa msanii ambaye anatoa ngoma chache sana kila mwaka huku kila ngoma akiilenga iweze kumrudishia uwekezaji wake na kumaptia faida zaidi kama alivyowahi kunukuliwa akisema:

‘Muziki wangu naufanya kibiashara zaidi hivyo mashabiki wangu wanielewe pale ninapochelewa kutoa ngoma’.

Bado haijajulikana ni siku gani staa huyo ataachia video ya ngoma hiyo.

 

Jux: WIVU ni confession kwa Vanessa Mdee?
Jux: WIVU ni confession kwa Vanessa Mdee?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *