Aliyekuwa mke wa Marehemu mzee Nelson Mandela, Winnie Madikizela-Mandela amekosoa vikali uongozi wa chama tawala cha taifa hilo ANC.

Winnie ambaye alipigana vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo amesema kuwa taifa hilo kwasasa linakabiliwa na matatizo makubwa yanayosababishwa na chama tawala cha ANC kinachoongozwa na rais wa sasa Jacob Zuma.

Winnie amesema kuwa kuna vitu vingi ambavyo vimefanywa kimakosa na kwamba chama hicho kinahitaji uongozi mpya ili kushirikiana na viongozi wazee wa chama.

Rais Zuma
Rais Zuma

Pia amelalamikia kuhusu ufisadi nchini humo na kuongezea kwamba sasa ni wakati wa watu kujichunguza.

Matamshi yake yanajiri wakati ambapo mirengo tofauti ya chama hicho inakabiliana kuhusu kuimarisha uungwaji mkono wa chama hicho baada ya matokeo mabaya ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *