Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeufungia wimbo mpya wa Nay wa Mitego ‘Wapo’ kutokana na kukosa maadili kwa jamii.

Nay wa Mitego amekamatwa na Jeshi la Polisi kutokana na wimbo huo ambapo inasemakana kuiimba Serikali ya iliyopo madarakani.

Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa, Godfrey Mngereza amesema ni marufuku wimbo huo kupigwa sehemu yoyote kutokana na maudhui mabaya ya wimbo huo.

Katibu huyo amesema kuwa “Tunatangaza rasmi kuufungia wimbo mpya wa Nay wa Mitego, huu wimbo hauna maadili, marufuku hii siyo kwa redio pekee au runinga, kwenye mitandao ya kijamii, kuna mamlaka ambazo zinasimamia hilo kwa hiyo wananchi wanatakiwa kuwa Maliki,”.

Pia amesema kwa sasa baraza hilo litamwita rappa huyu kwajili ya mahojiano na kutoa adhabu nyingine kutokana na huyo kurudia kosa hilo mara kwa mara.

Baraza hilo kama likimwita mwanamuziki huyo itakuwa mara ya pili baada ya mwaka jana kuitwa na kufungiwa kwa nyimbo yake kutokana na kukosa maadili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *