Wimbo wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz uitwao Yatapita imefanikiwa kufikisha Streams Milioni 10 kwenye BoomPlay Tanzania na Views Zaidi ya Milioni 11 kwenye upande wa Video ambao ni Youtube.

Haya ni mafanikio mengine kwa wimbo huu wa Diamond wenye wiki chache sokoni lakini unafanya vizuri kutoka na ubora wa wimbo huo.

Kwa Views Milioni 11 ndani ya wiki 3, Yatapita ndio wimbo uliotazamwa zaidi mwaka 2023 Afrika Mashariki kuliko wimbo wowote ukanda huu.

Hiyo sio mara ya kwanza kwa Diamond kufanya hivyo kwani alishawahi kufanya hivyo katika nyimbo zake mbali mbali alizotoa hapo awali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *