Kingo wa Arsenal, Jack Wilshere amesema hatoshangazwa na mashabiki nchini Uingereza endapo watafikia hatua ya kuwazomea wachezaji waliokuwa wanaunda kikosi cha nchi hiyo katika fainali za Euro zilizofanyika Ufaransa.

Wilshere amesema anatarajia suala hilo kujitokeza kwenye baadhi ya mechi za ligi kuu nchini Uingereza inayotarajiwa kuanza Agosti 13 mwaka huu katika viwanja tofauti nchini humo.

Kiungo huyo amesema kama ikitokea wakazomewa mashabiki wana haki ya kufanya hivyo kutokana na timu yao ya taifa kufanya vibaya katika mashindano ya Euro mwaka huu tofauti na mashabiki walivyoitarajia timu hiyo.

Wilshere amesema mashabiki wengi wanataka kutumia nafasi hiyo kuonyesha hasira zao kwenye mechi za ligi kuu kutokana na kukaa kimya toka timu hiyo itolewe kwenye mashindano hayo

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa wanaunda kikosi cha Uingereza kilichoshiriki mashindano ya Euro na kutolewa na Iceland kukapelekea kocha wa wakati huo Roy Hudgso kuachia ngazi kuinoa timu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *