Did the HIP HOP miss JAY MOE? Sooner than later we will get to know. Mkali na legendary wa Hip Hop, Juma Mchopanga a.k.a Jay Moe ANAREJEA TENA. Haijulikani iwapo nae ANAAMKA TENA au yeye HAKULALA KABISA lakini kila kitu kitathibitika kwenye ngoma yake mpya ya PESA YA MADAFU. Kwa miaka takribani minne staa huyo kutoka kundi la WATEULE linaloundwa na mastaa wengine, SOLO THANG, MCHIZI MOX na JAFFARAI amekuwa kimya huku akiusoma mchezo mpya wa Bongo Fleva unavyokwenda hususani kwenye eneo lake la HIP HOP.

10957375_366249356887612_703175986_n

Jay Moe anarudi huku muziki wa sasa ukiwa unamfahamu staa mpya, Ney wa Mitego na wengineo.

Je? Mzee wa NATAKA DEMU ataweza kumpata DEMU amtakae kwa wakati huu? Jambo moja ambalo ni HAKIKA kwa watu wanaomjua Jay Moe, ni kuwa Jay Moe ni NATURALLY TALENTED RAPPER, na sifa zake za wazi uwezo wake mkubwa wa kuandika mashairi ambayo ukiyasikiliza wakati uko kwenye daladala na unaelekea nyumbani unaweza kukubali kupitiliza kituo unachopaswa kushuka ili tu umsikilize hadi mwisho. Pia ni msanii ambaye aina yake ya kufikisha mashairi hayo, style yake ya ku-rap inaofautiana sana na wana HIP HOP wengine na mwisho UTUNDU wa ubunifu wa matumizi ya maneno na matamshi ni sifa ya ziada na ndio maana kabla ya kuitwa Jay Moe, kwanza aliitwa Moe Flavor!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *