Klabu ya West Ham imekataa ofa ya tatu ya paundi milioni 22.5 kutoka Marseille kwa ajili ya kumsajili kiungo wao Dimitri Payet ambaye anataka kuondoka kwenye timu hiyo.

West Ham wapo tayari kumuachia kiungo huyo kwa ada ya uhamisho yenye thamani ya paundi milioni 30 ndiyo watamuachia mchezaji huyo.

Payet mwenye umri wa miaka 29 ameonyesha nia ya kuondoka na kurudi kwenye timu yake ya zamani ya Marseille kwa sababu za kifamilia ambapo kwasa anaendelea kufanya mazoezi na timu ya vijana ya West Ham wenye umri chini ya miaka 23.

Kiungo huyo amejiunga na West Ham mwaka 2015 kutoka Marseille kwa ada ya uhamisho iliyogharimu paundi milioni 10.

West Ham wameshinda mechi mbili za ligi kuu nchini Uingereza bila mchezaji huyo ambaye ni mcheaji bora wa klabu hiyo msimu uliopita.

Toka atue West Ham amecheza mechi 60 na kushinda magoli 15 toka alipojiunga na wagonga nyundo hao wa London.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *