Nahodha wa Leicester City, Wes Morgan amesaini mkataba mpya na mabingwa hao wa Uingereza ambapo utamuweka kwenye klabu hiyo mpaka mwezi Juni 2019.

Beki huyo mwenye miaka 32 amecheza kila mechi kwenye ligi msimu uliopita na kuisaidia Leicester City kushinda taji la ligi kuu nchini Uingereza.

Morgan alijiunga na Leicester City akitokea Nottingham Forest Januari 2012 na amecheza mechi 182 za ligi kwenye klabu hiyo yenye maskani yake King Power studium.

Kwa upande mwingine kocha wa Leicester City,  Claudio Ranieri amemuelezea Morgan kama kiongozi na shujaa wa timu hiyo na kusema pia klabu ilikuwa bado inahitaji huduma yake.

Vile vile mshambulia wa klabu hiyo, Jamie Vardy alishasaini mkataba mpya baada ya dili la kwenda Arsenal kushindika lakini kiungo N’Golo Kante amejiunga na Chelsea kwa ada ya uamisho ya paundi milioni 30 na kunatetesi kuwa Riyad Mahrez anaondoka kwenye timu hiyo.

Morgan: Akishangilia na wachezaji wenzake wa Leicester City moja ya goli lake alilofunga katika mechi ya ligi kuu nchini Uingereza
Morgan: Akishangilia na wachezaji wenzake wa Leicester City moja ya goli lake alilofunga katika mechi ya ligi kuu nchini Uingereza

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *