Wenyeviti wa Serikali za mitaa na vijini nchini wameruhusiwa kutumia mihuri ya serikali kama zamani wakati serikali inaendelea kutafuta namna sahihi watakavyoitumia mihuri hiyo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), George Simbachawene wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu suala hilo.

Simbachawene amesisitiza kuwa serikali inatambua kuwa viongozi wa serikali za mitaa ndiyo nguzo za utendaji wa serikali na kwamba serikali ilikuwa haikuzuia kutumia mihuri hiyo.

Waziri huyo ameendelea kusema kuwa haikuwazuia wenyeviti kutumia mihuri hiyo bali ilikuwa imesitisha kutokana na baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa kutokuwa waaminifu kwa kusainisha mikataba mikubwa ya ardhi tofauti na sheria inavyosema.

Mkutano huo  na wanahabari pia ulihudhuriwa na baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa ambao kabla ya tamko hilo walikuwa wamepanga kwenda mahakamani kwa ajili ya kufungua kesi juu ya kutafuta vifungu vinavyowakataza kutokutumia mihuri hiyo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *