Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema waamuzi nchini Uingereza wanalindwa kama simba kwenye kituo cha kuhifadhi wanyama.

Wenger amesema hayo baada ya mechi ya ligi kuu kati ya Arsenal dhidi ya Manchester City ambapo City walishinda 2-1.

Kocha huyo amesema kuwa maamuzi mabaya ya refa ndiyo yalisababisha timu yake kupoteza mchezo huyo dhidi ya Manchester City.

Arsenal ndiyo walianza kuongoza kwa goli la dakika za mapema lililofungwa na Theo Walcott baada kupokea pasi maridani kutoka kwa Alexis Sanchez.

Goli la kwanza la Manchester City lilifungwa na Leroy Sane licha ya kanda za video zinaonyesha alikuwa ameotea kidogo.

Pia Wenge amesema kuwa David Silva alikuwa ameotea wakati Raheem Sterling alipofunga goli la pili na la ushindi wa City.

Hata hivyo si wazi iwapo alingilia uchezaji wa kipa Petr Cech.

Wenger alisema alisema “Nataka walindwe vyema, na nataka wahakikishiwe usalama wao, lakini iwapo wangekuwa wanafanya maamuzi sahihi, ingekuwa hata bora zaidi.”

Pia aliongeza Aliongeza: “Ninaelewa kwamba City wanaonekana kuwa furaha sana hata mimi ningefurahi Β lakini nafikiri mabao hayo yalikuwa ya kuotea.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *