Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kwamba hatma yake katika klabu hiyo ya Emirates inategemea jinsi matokeo ya klabu hiyo msimu huu yatakavyokuwa.

Wenger amesema kwamba mkataba wake utakamilika Juni mwakani kwa hivyo atakachofanya baada ya hapo itategemea na matokeo ya msimu huu kama kuendelea au kuachia ngazi.

Kocha huyo ambaye ni raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 66, aliajiriwa kama kocha wa Arsenal mwezi Septemba mwaka 1996 kuingoza klabu hiyo.

.

Arsenal haijashinda taji la ligi kuu ya Uingereza tangu mwaka wa 2004 jambo ambalo limechochea uhasama dhidi ya Wenger haswa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Awali wenger alikuwa amehusishwa na wadhfa wa kocha wa timu ya Uingereza lakini Sam Allardyce akachaguliwa kuwa kocha wa timu hiyo.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *