Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekubali kuachia klabu hiyo mwisho wa msimu huu baada ya kufanya vibaya.

Maamuzi ya kocha huyo yanakuja baada ya kufikiana na uongozi wa timu hiyo kutokana na mwenendo mbaya kwenye klabu hiyo.

Arsenal kwasasa ipo nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza na wanaweza kushindwa kuingia nafasi nne za juu kwa mara ya pili mfululizo.

Wenger mwenye umri wa miaka 68 ameshinda makombe matatu ya ligi kuu nchini Ungereza pamoja na vikombe 7 vya FA.

Kocha amewashukuru mashabiki pamoja na viongozi wa klabu hiyo kwa upendo waliomuonesha wakati akifundisha timu hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *