Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa  bado klabu inaweza kushinda taji la ligi kuu nchini Uingereza msimu huu licha ya tofoutiyla pointi 12 kati yake na Chelsea.

The Gunners, ambao kwa mara ya mwisho walishinda taji la ligi kuu mwaka 2004 wameshuka hadi nafasi ya 4 baada ya kufungwa 3-1 na Chelsea Jumamosi iliopita.

Timu hiyo mwishoni mwa wiki kinaialika Hull City katika uwanja wa Emirates baada ya kupoteza mechi nne kati ya tisa ilizocheza.

Wenge amesema ”Bado hatujasalimu amri”, alisema raia huyo wa Ufaransa.”Hata iwapo unadhani tumeshafanya hivyo, mimi bado sijasalimu amri-hatuweza kufikiria hivyo”.

Kwa sasa ni pointi tano pekee zinazotenganisha Tottenham ilio nafasi ya pili na Manchester United iliopo katika nafasi ya sita.

Pia Wenger ameongeza kwa kusema kuwa tuko katika eneo ambalo ni gumu sana na ugombeaji wa kila nafasi ni muhimu sana msimu huu ikilinganishwa na ule uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *