Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesaini mkataba mpya wa miaka miwili katika klabu hiyo baada ya kufikiana makubaliano.

Wenger na mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke walikutana Jumatatu kuamua hatima ya meneja huyo na kisha uamuzi wao ukawasilishwa kwa mkutano wa bodi jana.

Arsenal walimaliza Ligi ya Premia wakiwa nafasi ya tano ikiwa ni mara ya kwanza kumaliza chini ya nafasi ya nne tangu Wenger alipojiunga nao mwaka 1996.

Wenger aliongoza Gunners kushinda mataji matatu ya Ligi ya Premia na pia vikombe vinne vya FA misimu yake tisa ya kwanza kwenye usukani.

Mwaka 2003-04, aliibuka meneja wa kwanza tangu 1888-89 kuongoza timu iliyomaliza ligi kuu bila kufungwa.

Lakini baada ya kushinda Kombe la FA mwaka 2005, walisubiri kwa miaka mingine tisa kabla ya kushinda kikombe kingine.

Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakimtaka Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 67 ajiuzulu, hasa baada ya matokeo mabaya msimu huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *