Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa timu yake ina nafasi ya kunyakuwa ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza msimu huu kutokana na kiwango chao kuwa bora.

Arsenal kwa mara ya mwisho kutwaa taji hilo ilikuwa mwaka 2004 ambapo walitwaa bila ya kupoteza mechi yeyote.

Wenger mwenye umri wa miaka 67 amesema kuwa mshindi wa taji la ligi kuu atakuwa na pointi 82 na 86 mwaka huu.

Wenger ameongeza kwa kusema kuwa kwasasa wapo katika nafasi nzuri zaidi ya kuwania taji la ligi ya Uingereza ikilinganishwa na miaka mitano au sita iliopita.

Wenger amesema kuwa anafikiri kwamba anahitaji pointi 62 kutoka kwa mechi 29 zilizosalia kushinda taji.

Arsenal ni wa pili katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa ni mojawapo ya timu tatu zenye pointi 20 na wako katika nafasi ya pili kutokana na tofauti ya mabao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *