Chama cha soka nchini Uingereza (FA) kimemfungulia mashitaka ya utovu wa nidhamu kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kwa madai ya kumkashifu refa na kumsukuma mwamuzi wa akiba.

Kocha huyo alimsukuma mwamuzi wa akiba, Anthony Taylor na kutumia lugha mbaya katika mechi ya ligi kuu ya nchini humo dhidi ya Burnley ambapo Arsenal ilishinda 2-1 kwenye mchezo huo.

Mara baada ya mchezo huo kumalizika Wenger aliomba radhi kwa kitendo alichofanya kilichopeleka kutolewa nje ya eneo ambalo huwa wanasimama makocha.

FA imempa kocha huyu mpaka muda mpaka siku ya Alhamisi saa 3 usiku awe amewasilisha utetezi wake juu ya mashtaka hayo.

Hata hivyo Marefa wastaafu wa England, akiwemo Keith Hackett na Howard Webb, wametaka kocha huyu kupewa adhabu ya Kifungo kisichopungua michezo sita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *