Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa umaarufu mkubwa alionao umemfanya kushindwa kufanya vitu vingi ambavyo kama binadamu na yeye alitamani kufanya.

Akiwa hajawahi kupanda daladala kwa miaka 11 sasa, tangu alipovikwa taji la Miss Tanzania mwaka 2006.

Wema amesema kuwa akiwa ndani ya gari lake barabarani hujisikia raha sana kuona watu wakiwa wamepanda daladala wakiwa wanazungumza na kucheka, kitu ambacho anakimiss sana, lakini hamna namna anayoweza kufanya.

Wema amesema kuwa “Unajua kiukweli kabisa natamani mno kupanda daladala, kwa sababu hata mimi ni binadamu, kuna kipindi natamani kupanda gari kutoka kwangu mpaka Kariakoo au mpaka Mbagala, lakini unafikiria utakapopanda itakuwa ni vurugu na siyo starehe tena, huu umaarufu kwa kweli unani-’cost’ sana wakati mwingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *