Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam linaendelea kuwashikilia mastaa wawili wa Bongo Fleva, Nyandu Tozi na Khaleed Mohamed a.k.a TID pamoja na mastaa wengine wa wakubwa akiwemo Wema Sepetu na Babuu wa Kitaa kwa kashfa ya UNGA.

Ingawa bado haijajulikana endapo mastaa wengine waliohojiwa na polisi ‘wamemalizana’ au upelelezi zaidi unaendelea lakini kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro, mastaa kadhaa akiwemo Wema Sepetu bado wako chini ya ulinzi wa jeshi hilo.

Sakata la kuhojiwa kwa wasanii hao lilianza baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuweka wazi majina ya wasanii wanaodhaniwa wanahusika kwa namna moja au nyingine na wimbi la uuzwaji, utsambazwaji na utumiwaji wa dawa za kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *