Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu kupitia akaunti yake Instagram amesema anatajia kuachia filamu mpya ‘Heavesent’ akiwa na muigizaji mwezake Gabo Zigamba.

Wema Sepetu ambaye yupo kimya kwenye filamu ameweka picha ambayo ni sehemu ya movie hiyo akiwa na Gabo Zigamba pamoja na kuandika maneno yenye maana ya sababu ya kukuatana na Gabo kwenye movie hiyo.

Wema Sepetu pamoja na Gabo, wako mbioni kuachia filamu hiyo “Heavensent” ambayo itakuwa bora zaidi.

Muigizaji huyo ameahidi kwamba muda huu sio wa mchezo tena, amekuja kuwapa wa Tanzania kitu ambacho siku zote walikuwa wakikihitaji katika tasnia ya filamu hapa Bongo.

Katika filamu hiyo ya “Heavensent” ambayo imeongozwa na  Neema Ndepanya chini ya kampuni ya Fontana Entertainment, Wema Sepetu aliamua kushare baadhi ya picha za Scene ya filamu hiyo huku akiwaahidi watanzania mambo mazuri kutoka kwake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *