Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ni miongoni mwa wanachama wapya waliotambulishwa kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo.

Kupitia taarifa ya Chama hicho imesema kuwa baada ya kesi ya kikatiba kuwasilisha mahakamani leo Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe anatarajia kuwakaribisha wanachama wapya akiwemo Wema Sepetu.

Picha zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zinamuonesha Wema akiwa mahakamani pamoja baadhi ya wanachama wa Chadema akiwemo mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe pamoja na Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya wakiwa mahakamani huku akionesha ishara ya alama ya Chadema.

Ikumbukwe kuwa Wema Sepetu alikuwa akimpigia kampeni Makamo wa Rais Samia Suluhu (CCM) kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo alizunguka nae mikoa yoye ya Tanzania akimnadi.

Wema Sepetu ni miongoni mwa wasanii waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akijihusisha na masuala ya dawa za kulevya ambapo kesi yake inaendelea katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *