Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu amesema kuwa filamu yake ambayo amefanya na muigizaji kutoka Ghana Van Vicker itatoka mwaka huu mara baada ya kukamilika.

Wema Sepetu amesema kuwa kinacho ikwamisha kazi yake hiyo isitoke ni muigizaji Van Vicker kuwa na ratiba nyingi ambazo zinapelekea asindwe kurekodi vipande vyake kwa wakati.

Van Vicker alikuja nchini miaka miwili iliyopita kwaajiri ya kufanya filamu ya marikia huyo ambayo Wema Sepetu aliweka wazi jina la filamu hiyo kuwa itaitwa ‘Day After Death.’

Kwa sasa wema ameachia filamu mpya inayoitwa ‘Heaven Sent’ filamu ambayo haijaanza rasmi kupatikana mtaani na kwa sasa inapatikana kwenye ‘Aplication’ yake ya Wema Sepetu Mobile Aplication.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *