Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu amewataka mashabiki wake wamuombee ili apate mume bora atakayekuwa na heshima.

Wema amesema kuwa mume huyo anayemtaka yeye asiwe mtu maarufu kama walivyokuwa wanaumeume zake wa zamani.

Muigizaji huyo amewataka mashabiki zake wamfariji katika suala la kutafuta mume na siyo kumhusisha kila mara na uhusiano wa kimapenzi Diamond.

Wema amesema hayo wakati akimjibu shabiki katika kurasa wake wa Instagram, na kumtaka atambue Diamond ni baba wa watoto wawili kwa sasa na ifike kipindi watu waamini kwamba hakuna kinachoendelea kati yao.

Wema amemjibu kama ifuatavyo shabiki huyo “Sasa baby aliokwambia namtaka Damond ni nani? Life has to go on, yule ni baba wa watoto wawili jamani. Its about time u guys accept that me and Naseeb no more. Mnachotakiwa kuniombea ni nipate mwanaume bora na siyo bora mwanaume na mwenye heshima zake,”.

Muigizaji huyo hivi karibuni alikutana na Diamond katika sherehe ya siku ya kuzaliwa ya Sallam na kupiga picha ambazo zilizua gumzo huko mitandaoni kutokana na ukaribu wao siku hiyo.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *