Malkia wa Bongo movie, Wema Sepetu ‘ Madam’ mara nyingi upendelea kusafiri nchi mbali mbali dunia ikiwa ni kuimarisha kazi zake za sanaa au kwenda kupumzika kwa mara moja kutokana na skendo zinazokuwa zinamkabili staa huyo.

Staa huyo ameonekana akisafiri nchini Dubai huku watu wakijiuliza kwanini amesafiri nchini humo au kuna kitu gani kinaendela nchini Dubai au amekwenda kutangaza kazi zake zijazo au la.

Wakati akielekea Dubai Wema Sepetu alisindikizwa na mashabiki kibao waliokuwepo uwanjani hapo huku yeye mwenyewe akionekana ni mtu mwenye furaha baada ya kuona watu wengi kumsindikiza.

Wema Sepetu: Akiwa uwanja wa ndege kwa ajili ya kusafiri Dubai.
Wema Sepetu: Akiwa uwanja wa ndege kwa ajili ya kusafiri Dubai.

Watu wanajiuliza kwanini baadhi ya mastaa wa Bongo upendelea kusafiri sana kuliko kukaa nchini kwao au kunafaida wanaipata wakati wakisafiri au kuna biashara nyingine inafanyika kinyume na kazi zao za sanaa?

Nchi ambazo mastaa wa Bongo upendelea kusafiri mara kwa mara ni Afrika Kusini, China Dubai pamoja na nchi za Ulaya japokuwa siyo sana.

Baadhi ya wadadisi wa mambo wanasema kuwa uhenda mastaa hao ufanya biashara haram au kwenda kujiuza nchi hizo lakini hakuna ushahidi wa kutosha kuhusu masuala hayo japokuwa kuna baadhi ya mastaa wa Tanzania wamekamatwa na madawa ya kulevya na hivi sasa wanatumikia vifungo.

775146ad-7de2-4184-a718-9d53c8059853

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *