Muigizaji wa Bongo Movies, Wema Sepetu leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dae es Salaam kwa kosa la matumizi na kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi.

Wema alipandishwa kizimbani akiwa na wenzake wawili, Matilda Abass na Angelina Msigwa ambao ni wafanyakazi wake wa ndani.

Muigizaji huyo amekana makosa yote na Mahakama imeahirisha kesi hiyo mpaka itakaposikilzwa tena Julai 14, mwaka huu.

Katika kesi hiyo Wema na mwenzake wanakabiliwa na makosa matatu yanayohusiana na matumizi ya madawa ya kulevya aiana ya bangi.

Wema Sepetu ni miongoni mwa wasanii wa Bongo waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanaotumia dawa za kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *