Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu leo amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi.

Kesi hiyo imeshindwa kuendelea tena leo baada ya Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Thomas Simba kutokuwemo mahakamani.

Wema amekana mashataka hayo na hivyo kesi yake kusogezwa mpaka tarehe 1 mwezi wa nane ambapo itaanza kusikilizwa.

Muigizaji huyo na wenzake anatuhumiwa kwa kesi ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi.

Wema ni miongoni mwa wasanii nchini waliotaja na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakijihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *