Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu amewachana baadhi ya watu wanaomtolea matusi muigizaji mwenzake, Aunt Ezekiel baada ya kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya Zari.

Wema amesema unatakiwa ufike wakati watu waelewe na waongozwe kwa akili zao za kuzaliwa kwa sababu hakuna kitu kibaya ambacho amekifanya Aunt, kwa kuwa staa mwenzake huyo kwa sasa ni mmoja wa familia hiyo.

Muigizaji huyo maarufu kama Madam amewataka watu hao wamuache Aunt kwani hana kosa lolote hata kama angekuwa yeye asingeweza kuacha kwenda kwa sababu tayari ni familia na hawezi kumuacha mumewe aende peke yake.

Pia Wema ameongeza kwa kusema kuwa anachukizwa sana na jinsi watu hao  wanavyomrushia maneno ya kashfa Aunt Ezekiel kwenye mitandao ya kijamii kwani si tabia nzuri.

Mwezi uliopita Aunt Ezekiel aliudhuria sherehe ya kuzaliwa ya Zari The Lady iliyofanyika visiwani Zanzibar akiongozana na mpenzi wake Moses Iyobo ambaye ni mcheza show wa Diamond Platnum.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *