Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ameamua kutumia siku ya Wanawake Duniani kushiriki katika zoezi la upandaji miti mkoani Morogoro leo.

Kupitia akaunti yake ya Instagram Wema Sepetu ameweka picha akiwa na mbunge wa viti maalum (Chadema) mkoani Morogoro, Devetha Minja pamoja na wanawake weningine.

Wema akiwa na wanawake leo mkoani Morogoro wakipanda miti.
Wema akiwa na wanawake leo mkoani Morogoro wakipanda miti.

Wema ambaye amehamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akitokea CCM mwezi uliopita yupo mkoani Morogoro kwa kushughuli zake binafsi.

Muigizaji huyo ameungana na wanawake wa Mkoa wa Morogoro kuadhimisha siku hii kwa kupanda miti kwa lengo la kupunguza joto na kero ya maji hapo baadaye.

Pia Wema ameendelea kuwahimiza mashabiki wake wamuite Kamanda, jina  alilojibandika  baada ya kukabidhiwa kadi ya chama hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *