Muigizaji wa Bongo movie, Wema Sepetu ameendelea kusota rumande akisubili uchunguzi ukamilike kwa tuhuma za kukutwa na misokoto ya bangi pamoja na karatasi za kusokotea ‘Lizla’.

 

Wema anatarajia kufikishwa mahakamani kuanzia muda wowote baada ya uchunguzi wa kesi yake kukamilika.

 

Wasanii wenzake jana walifikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kesi yao ya kujihusisha na madawa ya kulevya ambao wamepewa dhamana baada ya kukidhi vigezo vya dhamana.

 

Wasanii waliofikishwa mahakamani hapo jana ni Khalid Mohamed (TID) Hamidu Chambuso (Nyandu Tozy), Babuu wa Kitaa, Romy Jones, Tunda, Lulu Diva na Recho.

 

Wasanii hao walitajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kujihusisha na uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *