Muigizaji wa Bongo Movie, Wema Sepetu ameachiwa kwa dhamana katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam baada ya kukidhi vigezo vya dhamana hiyo.

Wema Sepetu leo amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka matatu ambayo yote yanahusiana na uvutaji bangi baada ya kukamatwa wiki iliyopita.

Wema na wenzake hao wamekana mashtaka hayo na kuruhusiwa kupewa dhamana ya shilingi milioni 5 kila mmoja pamoja na kuwa na wadhamini wawili kila mtuhumiwa.

Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro jana amesema kuwa jeshi hilo linamshikilia Wema na wenzake saba ambao walikamatwa na vielelezo.

Wema ni miongoni mwa wasanii waliotajwa n mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanaojihusisha na na matumizi ya dawa za kulevya ambao walitakiwa kuripoti kituo cha polisi jijini Dar es Salaam.

Picha kwa hisani ya Global Publishers

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *