Muigizaji nyota wa Bongo movie, Wema Sepetu ameamua kuifutilia mbali kundi la team Wema katika mitandao ya kijamii kwa madai wao ndio chanzo cha matatizo mengi katika maisha yake kwa ujumla.

Wema amedai amekuwa hana amani kwa ajili ya team Wema kutokana na kumgombanisha na baadhi ya waigizaji wenzake pamoja na jamii inayomzunguka ambapo team hiyo huwa inazusha mambo ambayo Wema ayamuhusu.

Muigizaji huyo ambaye amejizolea sifa kibao kwenye soko la filamu kutokana na uigizaji wake ndani ya movie zake alizowahi kuigiza mara baada ya kujikita rasmi katika sanaa ya maigizo.

Muigizaji huyo amesema kuwa “Sasa mimi naomba kusema kitu kimoja, naomba kuanzia sasa hivi sitaki kuijua team Wema, kwa sababu sielewagi team Wema ilitokea wapi, mimi sijui na sio chanzo cha team Wema na sijui mmetokea wapi mmekuja kuniharibia maisha yangu,”.

Katika siku za karibuni katika mitandao ya kijamii kumeibuka vitendo kwa wasanii na watu maarufu kuwa na team, team ambazo huwa zinawasapoti katika kazi zao mbali mbali lakini baadhi ya team huwa zinasababisha marumbano baina ya msaani kwa msanii.

Team ambazo ni maarufu katika mitandao ya kijamii ni Team Wema ambayo kwasasa mwenyewe kaifuta, Team Diamond Platnumz, Team Kiba pamoja na team Kajala hizo ni team ambazo zinasumbua sana katika mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *