Staa wa filamu nchini, Wema Sepetu amempa hongera Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tannzania, John Pombe Magufuli kwa kuwakuza vijana wengi kiakili na ufahamu kutokana na namna anavyoongoza nchi na kuleta tija kwa watanzania wote.

Pongezi hizo  za Wema Sepetu zimekuja ikiwa ni takribani miezi tisa sasa toka Rais Magufuli kutangazwa na kuiongoza Tanzania.

MAGUFULIBEST

Staa huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema katika serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli yenye kauli mbiu ya ‘Hapa kazi tu’ ni lazima vijana wafanye kazi na kuachana na mambo yasiyo na msingi katika jamii.

Wema Sepetu aliandika maneno haya kwenye akaunti yake ya Instagram “Serikali ya ‘Hapa kazi tu’ inatakiwa ikukuze kiakili na ufahamu kuwa miaka haiendi nyuma bali inasonga mbele. Dr John Pombe Magufuli asante kwa kutukuza. Huu ni muda wa Kazi tu maneno maneno tuwaachiage watoto wadogo”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *