Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu amefunguka na kusema kuwa kwake jambo la kuimba muziki limeshindikana.

Wema amesema yeye hana mpango wa kuingia kwenye muziki, na hata wimbo wa Haitham alioshirikishwa hakuimba, lakini wamemgeuka na kuandika kwamba ameshirikishwa kuimba kwenye wimbo huo.

Amesema “Mi kuimba siwezi mwenzangu, kila nikijaribisha inabuma, ile nyimbo na Haitham umeshanisikia naipush, mi nafanyaga nilivyofanya halafau watu wananifanyia vitu vya ajabu, wananisaliti”.

Hivi karibuni msanii Haitham ameachia wimbo unaoitwa Play boy huku ukiandikwa ameshirikishwa Wema Sepetu, lakini hakuna mahali ambapo msanii huyo amesikika kuimba wala kurap na kuibua maswali mengi kwa wadau kwanini imekuwa hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *