Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu amewachana waigizaji wenzake wa Bongo Movie  baada ya kukaa kimya kuhusu suala la kupotea kwa Roma na wenzake.

Wema Sepetu kupitia akaunti yake ya Instagram amesema kuwa wasanii hao wanaposti picha wakiwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam wakizungumza masuala ya wakorea na Wafilipino bila kuulizia suala la Roma na Moni.

Ameandika haya kupitia Instagram:

By @wemasepetu
This Is Scary… Ni Janga kubwa sana kwa wasanii, kwa wananchi na Kwa Taifa letu kiujumla… Kinachonishangaza ni kuona baadhi ya wasanii wa Bongo movie wamekazana kupost eti wapo kwa Mkuu wa mkoa wakiongelea WaKorea na Waphilipino…. Mlikumbuka kumuuliza Mheshimiwa alipo Roma na Moni…???

Ameongeza kwa kusema “Au ndo mambo ya kila mtu anaangalia lake…. Au labda mpaka atekwe msanii wa Bongo movie pia ndo akili itatukaa sawa…??? Oh God help Us Please… Lakini pia wala sitoshangaa hata kama akitekwa msanii wa bongo movie hakuna atakaehangaika within Us zaidi ya wananchi peke yao na watu wetu wa karibu…

Pia amemalizia kwa kuandika “Tumejawa sana Unafki…!!! All in All namuonea sana huruma Nancy…. Our prayers are with u mama… Inshallah mumeo atapatikana… Tuzidi kumuomba Mungu…..??????…. Kabla sijasahau, Tuwage tuna hata fikra za kujua tupo kwenye wakati gani na tupost vitu gani….!!! Yaani mtu kapotea siku ya pili mko busy na kupost Wakorea na Waphilipino…?? SM.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *