Wanamuziki kutoka rekodi lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) wanatarajia kufanya show nchini Burundi siku ya tarehe 24 Septemba mwaka huu.

Kupitia ukurasa wake wa Intagram mmoja wa wananamuziki kutoka lebo hiyo Raymond ‘Rayvanny’ amesema kuwa watafanya show nchini humo ifikapo Septemba 24.

Show hiyo inatarajia kufanyika katika ukumbi wa Ecole Independente nchini Burundi ambapo kiingilio cha juu kitakuwa shilinigi 10,000 ya kitanzania.

Wasanii wanaounda lebo hiyo ni Rich Movoko, Raymond pamoja na Harmonize ambao ndiyo wanatarajia kufanya show nchini Burundi ili kuwapa burudani wakazi wa huko pamoja na kutangaza kazi zao mpya.

Wasanii hao pia wiki chache zilizopita walifanya show ya kufa mtu katika viunga vya jiji la Nairobi nchini Kenya ambapo walifanikiwa kuzoa mashabiki wengi katika show pamoja na kupata mapokezi ya hali juu nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *